688. Prophecy and Vision given to Raymond Aguilera on 16 February 1995 at 1:45 PM.

A Christian minister friend that I pray with came over to my house and told me he had just left the hospital. He is a volunteer chaplain there. He said that he tried to minister to an 83 year old Oriental man named Chan who had a broken leg. During his conversation with Mr. Chan, Mr. Chan revealed that he had made a promise to his grand parents when he was a child that he would never accept any religion. His grand parents told him that if he joined a religion that he would not be able to worship his ancestors. As my friend tried to minister to him and get him to know Jesus, he stated that he has kept that promise. Mr. Chan said, he would not accept anything because he was going to keep his promise to his grand parents.

So after telling me this story my friend seemed very disturbed for My minister friend is Chinese. He related to me how in the Chinese community, many Chinese people believe in worshipping their ancestors, and they have a hard time accepting Jesus Christ because of there belief of ancestor worshipping.

Well, we decide to pray for Mr. Chan. We had Communion and during the Communion prayer. I was praying in tongues and went into the spirit. Immediately during the prayer the Lord gave me a Vision/Prophecy. He showed me the same ball that I saw at the Full Gospel Business Men's Fellowship International Breakfast.

And the Prophecy was: "Beware of the cross on the ball, of the ball with the cross."

I was still in the spirit and praying when my tongue dialect changed. The next thing I saw was a vision of a large auger that is used to drill post holes. As I was watching this my friend began to pray to the Lord to open Mr. Chan's heart and to save him. As we were interceding for him all of a sudden I saw a scroll. And the scroll was being opened and my prayer language was just going crazy. Then I saw a Hand with a Pen spelling out C-H-A-N and the scroll was rolled back up.

Then the Lord said, "It is done."

I was watching this in the spirit as my friend prayed in English and I in tongues. Then we prayed against any curses on Mr. Chan and his family and to bring them to the Lord, and to do this through the Power of the Holy Spirit.

Then Lord showed me a kitchen faucet, but I was viewing it from underneath and as I watched, the water was turned on and I could see water coming out of the faucet.

And then the Lord said, "It is done."

Then my prayer language suddenly just stopped, but my friend just kept on praying. I stopped because the Lord stopped, but I could still sense, the Power, the Authority behind the Visions the Prophecies. I guess that's all. I don't know how the Lord is going to reach Mr. Chan or if He already has, but he is saved. I just don't understand some things, but I guess since He is God, He can do anything He wants, at any time He wants. That's all. (over)

Addition:

During this prayer in tongues I kept saying to the Lord in my mind, "I want this prayer be done with power, with the power of the Holy Spirit. You said in the Bible when two or more are gathered and in agreement that it would be done. And I want it done today! (over)

688. Unabii na Maono aliyopewa to Raymond Aguilera tarehe 16 Februari 1995, saa 7:45 mchana.

Rafiki yangu fulani katika Kristo ambaye ni mchungaji na ambaye huwa tunaomba naye, alikuja nyumbani kwangu nakuniambia kuwa yeye alikuwa anatoka hosipitali fulani. Na huko yeye ni mchungaji aliyejitolea pale ili kuhudumia. Aliniambia kuwa alikuwa amejaribu kumhubiria mzee mmoja wa miaka 83 wa kiume kutoka mashariki ya mbali. Yeye alikuwa anaitwa Chan ambaye amevunjika mguu. Wakati wa mazungumzo yake na Ndugu Chan, Ndugu Chan alimfunulia kuwa yeye alikuwa amefanya ahadi kwa mababu zake akiwa bado mtoto kuwa, kamwe asingelikubali dini nyingine yeyote. Mababu zake walimwambia kuwa kama atakubali dini nyingine yeyote, yeye asingeliweza kuwaabudi mababu zake. Wakati huyo rafiki yangu alipojaribu kumhubiria na kufanya amfahamu Yesu, yeye alisema kuwa yeye alikuwa ameihifadhi ahadi hiyo kwa uaminifu. Ndugu Chan akasema, yeye asingelikubali kingine kwa sababu, ilibidi yeye kutunza ahadi yake hiyo kwa mababu zake.

Kwa hiyo baada ya huyo rafiki yangu kuniambia historia hiyo, yeye alikuwa anaonekana kufadhaishwa sana kwa maana huyo rafiki yangu Mchungaji ni Mchina. Yeye alinieleza jinsi katika jamii ya Kichina wengi wao wanavyoamini ibaada ya kuwaabudu mizimu ya wazee wao waliokwisha kufa, na walikuwa wanapata shida sana kumkubali Yesu Kristo kwa sababu ya imani yao hiyo ya kuwaabudu mahoka au mizimu ya wazee wao.

Naam, sisi tuliamua kumwombea Ndugu Chan. Sisi tulikula Chakula cha Bwana (Komunio) na wakati wa maombi, mimi nilikuwa ninaomba katika lugha na kustukia niko kwenye ulimwengu wa kiroho. Mara na kwa ghafla Bwana akanipa Maono/Unabii. Yeye akanionyeshea mpira au tufe lile lile ambalo niliiona pale kwenye “The Full Gospel Business Men's Fellowship International Breakfast.”

Na Unabii ulikuwa: "Mjihadhari na msalaba uliokuwa kwenye mpira, au mpira uliokuwa na msalaba."

Mimi bado nilikuwa kwenye ulimwengu wa kiroho na huku nikiwa ninaomba mara nikakuta ndimi yangu ya maombi ikibadilika. Kilichofuata kukiona kilikuwa ni kekei kubwa sana ya kuchimbia nguzo. Wakati nikiwa ninaiangalia kekei hiyo, yule rafiki yangu akaanza kumwomba Bwana ili aufungue moyo wa Ndugu Chan na kumwokoa. Wakati tulipokuwa bado tunamwombea mara kwa ghafla nikaona karatasi kubwa sana iliyo viringishwa pande zote kama ile inayotumika katika maandiko ya kale. Na karatasi hiyo iliyoviringishwa ikifunguliwa na lugha yangu ya maombi ikawa inaenda kwa kasi kubwa sana. Kisha mimi nikaona mkono na kalamu ukiandika C-H-A-N na karatasi hiyo mara ikarudishwa.

Kisha Bwana akasema, "Imefanyika/imetimizwa."

Mimi nilikuwa ninaiangalia katika ulimwengu wa kiroho wakati rafiki wangu akiwa anaomba kwa lugha ya Kiingereza nami katika ndimi. Kisha tukaomba kuvunja laana yeyote iliyokuwa juu ya ndugu Chan na familia yake na kuwaleta kwa Bwana, na kufanya hivyo kwa njia ya Roho Mtakatifu.

Kisha Bwana akanionyeshea bomba la jikoni, lakini mimi nilikuwa ninaiangalia kutoka chini na wakati nikiwa ninaiangalia kutoka chini, maji yakafunguliwa nami nikaanza kuona maji yakiwa yanatiririka kutoka kwenye bomba hilo.

Na kisha Bwana akasema, "Imefanyika/imetimizwa."

Kisha lugha yangu ya maombi mara ikakoma kwa ghafla, lakini yule rafiki yangu akawa anaendelea tu na maombi. Mimi nilisimama kuomba kwa sababu Bwana alikuwa amekamilisha, lakini bado nilikuwa nahisi Nguvu, Mamlaka, nyuma ya Maono na Unabii huo.  Nadhani hayo ndiyo yote. Mimi sielewi ni kwa namna gani Bwana atakavyomfikia Ndugu Chan au kama tayari amekwisha kutana naye, lakini ninauhakika kuwa tayari amekwisha okelewa. Kwa kweli mimi sielewi mambo mengine, lakini nadhani kwa kuwa Yeye ndiye Mungu, Yeye anaweza kufanya lolote atakalo, wakati wowote atakao. Haya ni yote. (Mwisho).

Nyongeza:

Wakati wa maombi katika lugha nikawa ninaendelea kumwambia Bwana katika akili yangu, "Nataka maombi haya yafanyike kwa nguvu na uweza, kwa nguvu na uweza wa Roho Mtakatifu. Wewe ulisema katika Biblia wakati watu wawili au zaidi wakikusanyika na wakiwa katika makubaliano, yatafanyika. Nami nataka yafanyike leo hii! (Mwisho).

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.