|
832. Occurrence, Vision,
and Prophecy given to Raymond Aguilera on 22 November 1995 at 8:15 PM. During a Christian prayer meeting of about twenty plus people, the Lord showed me a small segment of Prophecy #154, and instructed me to tell this Occurrence. ************ >>>>>154. Prophecy, Vision, and Occurrence given to Raymond Aguilera on 12 July 1992 at 5:37 PM. I don't know.... I just don't know! I feel like I am right smack in the middle of a War. I just don't know whether to go on praying or to stand still or to hang it up. It's like you're in the middle of something beyond your comprehension. The Lord is showing me stuff. I see a vision of a Ram. No, it's two Rams. They are locking horns. They are hitting each others head extremely hard. I hear this sound echoing, as they're trying to crack each others skull. What does this mean?<<<<< ************* Almost three years later, I can still see and hear the two Rams hitting each others head extremely hard with the echoing sounds bouncing off the canyon's walls as they tried to crack each others skull. Vision: Then the next thing the Lord showed me was a large single Eye Ball looking down from Heaven. As I was looking at it, the eye somehow turned and looked down toward the earth.
Vision: Then I saw the Lord holding a SMALL American Flag. It looked like a toy flag, and He waved it in His left Hand.
Vision: All of a sudden a large bottomless Sink Hole appeared, and all kinds of objects started falling into it.
Prophecy: The next thing is extremely hard to explain because the Lord related to me that the United States was going to war. But the communication wasn't words or thoughts, He told my spirit directly, without words or by placing thoughts in my mind. I don't know how He did it, or how to explain it, other than what I have said. Comments: After I received this Occurrence-Prophecy, the Power Presence of the Lord was so strong that it left me shaken and overwhelmed. I had to leave the prayer meeting. At the present time, I am having a hard time keeping my balance in the flesh. I wish.., I knew how to explain all of this. It's almost like your spirit gets charged up and your physical body falls apart all at the same time. Your body feels like its going to explode from the inside out. It's not only physically exhausting, but you feel so alone. I mean totally ALONE!! There seems to be no one in the whole universe there except the Lord. That's great for your spirit, but your flesh is left in the middle of nowhere with no one there that could ever understand what you are experiencing. Somehow my body senses that it has no chance of living, and that it's doomed. I felt like.., just driving to some secret place and hiding. I guess.., I just wanted to be alone to think this out, but I had no place to go. At the present time, I am in overwhelming pain that is affecting my spirit. It's Thanksgiving morning, but I feel.., I am in the middle of nowhere. May the Lord Jesus Christ forgive us all. (over)
|
832. Matukio, Maono na
Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 22 Novemba 1995, saa 2:15 jioni. Wakati wa maombi kwenye kikundi cha maombi cha Wakristo chenye watu wapatao ishirini au zaidi hivi, Bwana alinionyeshea sehemu ndogo ya Unabii #154, na kuniagiza niwaambie kuhusu tukio hilo. ************ >>>>>154. Unabii, Maono na Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 12 Julai 1992 saa 11:37 jioni. Mimi sijui.... Kwa kweli mimi sijui! Najisikia kama mimi nimekwama katikati ya mapambano. Kwa kweli sielewi kama niendelee kuomba au kusimama tu wima au kuachia. Ni kama uko katikati ya kitu ambacho kiko nje ya ufahamu wako. Bwana ananionyeshea mambo ya ajabu. Naona maono ya Kondoo dume. Hapana ni madume mawili ya Kondoo. Wanapambana kwa pembe zao. Wanatwangana kwa nguvu zote. Nasikia mwangwi wa kishindo cha sauti ya kugonganisha vichwa vyao, kila mmoja akijaribu kuvunja kichwa cha mwenziwe. Hii ina maana gani? <<<<< ************* Baada ya kitu kama miaka mitatu baadaye, Mimi bado nilikuwa ninaweza kuona na kusikia wale Kondoo wawili dume wakitwangana vichwa kwa vichwa kwa kishindo kikubwa sana, na mwangwi wa vishindo hivyo vilikuwa vinagonga kwenye korongo fulani kubwa na kurudishwa na kingo za korongo hilo wakati wenyewe wakiwa kila mmoja wao akijaribu kupasua kichwa cha mwenziwe. Maono: Kisha kilichofuata ambacho Bwana alinionyeshea kilikuwa ni mtoto wa Jicho kubwa likiwa linaangalia kutoka Mbinguni. Hali mimi nikiwa ninaiangalia jicho hilo kwa namna fulani likajizungusha na kuangalia duniani.
Maono: Kisha nikamwona Bwana akiwa amelishikilia Bendera NDOGO ya Amerika. Ilikiwa inaonekana kama toyi au bendera zile za kuchezea watoto wadogo, naye akawa anaipungia kwenye Mkono wake wa kushoto.
Maono: Kwa ghafla shimo lisilo kuwa na mwisho la kuzamisha vitu likaonekana, na kila aina ya vitu vikatumbukia na kuzamia humo.
Unabii: Kilicho fuata kukiona ni kigumu sana kukieleza kwa sababu Bwana alinieleza kuwa Amerika ingelienda vitani. Lakini jinsi alivyo nieleza haikuwa kwa maneno au kwa mawazo, Yeye aliiambia roho yangu mmoja kwa mmoja, bila kutumia maneno au kuweka mawazo kwenye akili Yangu. Mimi sielewi jinsi alivyo fanya au jinsi ya kuiieleza kwa ufasaha, zaidi ya kile nilicho kisema. Ilani: Baada ya kupokea Tukio na Unabii huo, Nguvu za Uwepo wa Bwana ilikuwa ni mkubwa kiasi ambacho iliniacha mimi nikiwa ninatetemeka na kuzidiwa sana. Kwa wakati huu, ninapata shida kukaa kwenye mwili. Laiti… kama hata ningeliweza kujua njia ya kuyaeleza haya. Ni kama roho yako inatiwa nguvu sana na mwili wako unaishiwa na nguvu za kuhimili hayo; wakati huo huo. Mwili wako ni kama utaenda kulipuka kutoka ndani, ili ukatoke nje. Siyo kwamba ni kuchoka tu katika mwili, bali unajisikia kuwa mpweke sana. Namaanisha MPWEKE!! Kabisa. Ni kama kujisikia kuwa mpweke kiasi cha kujisikia kuwa hakuna kiumbe chochote katika ulimwengu wote huu, isipokuwa Bwana tu. Hili ni jambo kuu kwa roho yako, lakini mwili wako unaachwa katikati ya utupu ambao hakuna yeyote anayeweza kuuelewa kile unacho jisikia. Kwa namna fulani mwili wangu ulikuwa unapatwa na hisia ya kuwa hakuna uwezekaano wa kuendelea kuishi, na ya kuwa umeangamia. Mimi nilijisikia.., kutaka kwenda eneo la siri na kujificha humo. Nadhani…. Mimi nilitaka tu kuwa peke yangu ili kulifikiria jambo hili, lakini hapakuwa na mahala pa kwenda. Kwa sasa hivi, nipo kwenye maumivu yaliyo pindukia ambayo inaiumiza roho yangu. Ni siku ya kutoa shukrani asubuhi ya leo, lakini mimi ninajisikia…., nipo katikati ya mahala ambapo haipo. Naomba Bwana wetu Yesu Kristo atusamehe sisi na haya yote. (Mwisho). |
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )