|
850. Vision
given to Raymond Aguilera on 16 January 1996 at 8:30 PM. During praise and worship at a small church the Lord showed me one of those plastic thumb-tacks with a sharp point. Then the Lord said, "Look at the sharp point. Everything is going to come to a sharp point like this thumb-tack." Vision: Then as I looked around the small church in the spirit, I saw it being filled with people or images of people. One of the brothers later said that they were Angels. At first, I only saw three or four figures seated in the center of the church, and as the praise and worship progressed, the whole church began to be filled. I even saw these figures standing in the aisles all the way to the two exit doors. Like I said before, they looked like people, but they could have been Angels. This occurrence was not explained. Prophecy: Then later, the Lord said, "You're out of time. Don't build Me anymore churches." Vision: Then the Lord gave me a vision of a wooden cup. Then He dropped a white pearl inside the wooden cup, and said, "Save your pearls." Vision: Then the Lord gave me a vision of a fish. I could see the head and tail, but the center of the fish was missing. All that was holding the fish together was the bony spine. Then the vision stopped. Prophecy: Then during the worship one of the brothers prayed and said something about we invite you here or we welcome you Holy Spirit. Then the Lord said, "We WELCOME you!" But the way I received the Word from the Lord was as if the Lord was saying "We" are the center (Authority) not you. "We" welcome you, not you welcome US. Or in other words Jehovah, Jesus Christ, and the Holy Spirit welcome you into our PRESENCE not the other way around. |
850. Maono
aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 16 Januari 1996, saa 2:30 jioni. Wakati wa kusifa na kuabudu kwenye kikanisa ndogo, Bwana alinionyeshea mmoja ya zile kucha za bandia zinazo valiwa kwenye vidole vikiwa na ncha kali. Kisha Bwana akasema, "Angalia ncha ile kali, kila kitu kinaenda kwenye ncha hiyo kali kama ilivyo hiyo kucha bandia." Maono: Kisha wakati nikiwa naangalia kwenye kile kikanisa ndogo katika ulimwengu wa kiroho, mimi niliona kanisa hilo likiwa linajazwa na watu au vifuli vya watu. Mmoja wa ndugu baadaye akasema kuwa walikuwa ni Malaika. Mwanzoni, mimi niliweza kuona tu vifuli vya kitu kama watu watatu au wanne wakiwa wamekaa katikati ya kanisa, na wakati sifa na kuabudu ilivyo endelea, kanisa zima likaanza kujaa. Mimi hata nikaona vifuli vya watu wakiwa wamekaa kwenye uchochoro au korido hadi kwenye milango miwili ya kutokea. Kama nilivyo sema hapo kabla, walikuwa wanaonekana kama ni watu, lakini pia inawezekana kuwa ni Malaika. Tukio hilo sikuweza kupewa maelezo yake. Unabii: Kisha baadaye Bwana akasema, "Ninyi mmeishiwa na wakati. Msinijengee makanisa zaidi tena." Maono: Kisha Bwana akanipa maono ya kikombe cha mti au mbao. Kisha akatumbukiza lulu nyeupe ndani ya kikombe hicho cha mbao, na kusema. “Okoeni lulu zenu”. Maono: Kisha Bwana akanipa maono ya samaki. Mimi nilikuwa naweza kuona kichwa na mkia tu, na sehemu ya katikati ilikuwa haiko. Kile kilicho kuwa kinaunganisha samaki kichwa na mkia kilikuwa ni uti wa mgongo tu; ambao ni mifupa tupu. Unabii: Wakati wa kuabudu mmoja wa ndugu akaomba akisema kitu kuhusu kuwa tunawakaribisheni hapa au tunakukaribisha wewe Roho Mtakatifu. Kisha Bwana akasema, "Sisi TUNAWAKARIBISHENI ninyi!" Lakini jinsi mimi nilivyo ipokea Neno hilo kutoka kwa Bwana; ilikuwa ni kana kwamba Bwana alikuwa anasema "Sisi" ndio tunawakaribisheni (Sisi ndio Wenyeji, ndio tulio na Mamlaka) na wala siyo ninyi. "Sisi" tunawakaribisheni ninyi, na wala siyo ninyi Mtukaribishe Sisi. Au kwa maneneo mengine Yehova, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu wanawakaribisheni ninyi mbele ya UWEPO WAO na wala siyo kinyume chake. |
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )