|
866.
Visions and Prophecies given to Raymond Aguilera on 27 February 1996 at 8:15
PM. During worship the Lord showed me many visions so I will list them as I received them. Vision: I saw a large brick apartment complex which was covered with snow. As I was looking down at this complex I saw something flying down from the sky and heading for an open area in front of the complex. I fastened my eyes at this flying creature, and the Lord said, it was a Cherubim. After hearing this, I tried harder to see what this Cherubim looked like, but as looked, the Cherubim just faded in and out of focus in the spirit. For some reason the Lord would not let me focus in on the Cherubim. (over) Vision: Then the Lord showed me a heart. As I looked at the heart shape, it split open in the middle, and a water fall started pouring over the split heart sections. (over) Vision: The Lord showed me and enormous yellow-white sun with this pyramid in front of it. (over) Vision: I was shown this flying saucer flying in the air. Then I saw this kitchen faucet, but the pouring spout was facing up instead of down. The next thing I saw was this faucet spout as large as the saucer, but underneath the saucer, and when faucet was turned on; the flying saucer was pulverized. I found myself in the spirit an in the air and following another flying saucer flying over this green valley. Then somehow there appeared two of them flying side-by-side. As I watched them; they flew together (into each other) and became ONE saucer of the same size. Then out of nowhere the Lord's Fist came down from heaven with a POWERFUL FORCE and hit this flying disk dead center and knocked it straight down out of the sky. (over) Prophecy: The Lord said, "All that you see is True and Trustworthy." (over) Vision: The Lord showed me this dragon with it's tail moving slowly up and down almost like a whip. (over) Vision: I was shown two speed boats racing side-by-side over the water. (over) Vision: I saw the dragon's head again. (over) Vision: I saw this enormous volcano with hot molten rock inside. (over) Vision: The Lord showed me an upside down pyramid standing on it's vertex (or on it's point). (over) Vision: The Lord showed me this unusual looking hairy black spider with it's body split open. Then this blue-green turquoise colored body appeared from the center of the split body skin. (over) Prophecy: The Lord said, "See and learn." (over) Vision: Then I saw the heart shape again, but the heart was complete. As I watched, I saw a finger over the top of the heart, where the heart comes together. (over) Prophecy: Then the Lord said, "The Kingdom of God is before you." (over) Vision: I saw this wall of ice and it seemed to be moving. (over) Vision: I was shown two suspension bridges side-by-side. (over) Vision: Then I saw this large but almost flat bowl with a wooden flat stick laying across the center and over the top of the bowl. As I watched a lit white candle was placed in the center of the wooden flat stick which was over the center of the bowl. (over) Vision: I saw this large mountain which had a large arch carved out of the base. This arch was so big it went up about one third of the mountain. You could see right through the base of the mountain because of the arch, and in the center of this arched tunnel, a long board that went through the whole mountain was placed in the center of the arched tunnel. Now this board was used as a teeter-totter for I could see it move up and down, and it had some weights on each end. (over) Vision: The Lord showed me a black cast-iron frying pan filled with red hot coals. As I watched, the cast-iron pan was moved a few feet and the hot coals were poured into a big pot. This happened several times as I watched. (over)
|
866. Maono
na Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 27 Februari 1996, saa 2:15 usiku. Wakati wa kuabudu Bwana alinionyeshea maono mengi, kwa hiyo mimi nitayatoa kwa jinsi nilivyo ya pokea. Maono: Mimi niliona jumba moja kubwa lililo jengwa kwa matofali, likiwa limefunikwa na theluji. Wakati nikiwa ninaliangalia jengo hilo kwa chini, niliona kitu fulani kikiwa kinaruka kutoka juu angani, na kuelekea kwenda kutua sehemu fulani iliyo kuwa ya uwazi mbele ya jumba hilo. Mimi nikakaza macho yangu kwenye kiumbe hicho kilicho kuwa kinaruka, naye Bwana akasema alikuwa ni Cherubim. Baada ya kusikia hilo, mimi nikakaza macho yangu ili kuona sura ya huyo Cherubim, je anafananaje, lakini huyo Cherubim aliingia bila mimi kuiona sura yake sawa sawa na kuondoka katika Ulimwengu wa Kiroho. Kwa sababu fulani Bwana hakuniruhusu kumwona Cherubim huyo. (Mwisho). Maono: Kisha Bwana alinionyeshea moyo. Wakati nilipokuwa nayaangalia maumbile ya moyo huo kwa makini; mara moyo huo ukafunguka katikati na maporomoko ya maji yalianza kutokea na kuanza kuporomoka kupitia kwenye sehemu hiyo iliyofunguka ya moyo huo. (Mwisho). Maono: Bwana akanionyeshea jua ambalo lilikuwa kubwa sana; lenye rangi ya manjano-nyeupe kukiwa na piramidi fulani mbele yake. (Mwisho). Maono: Mimi nilionyeshewa sahani iliyokuwa inaruka angani. Kisha nikaona koki ya bomba la jikoni, lakini mdomo wa tepu ya bomba hilo ulikuwa unaangalia angani badala ya chini. Kilichofuata kilikuwa ni koki hiyo ya bomba ikivimba na kuwa kubwa kama sahani hiyo lakini ikiwa chini ya sahani hiyo, na pale koki hiyo ilipofunguliwa; sahani iliyokuwa inaruka, ilipondwa pondwa na kusagwa sagwa. Mimi nilijikuta niko kwenye ulimwengu wa Kiroho na huku nikiwa ninaifuatia sahani nyingine iliyokuwa inaruka juu ya bonde fulani iliyokuwa na rangi ya kijani kibichi. Kisha kwa namna fulani vikajitokeza visahani viwili vikiruka ubavu kwa ubavu. Wakati nikiwa ninaviangalia hivyo visahani viwili; vyenyewe vikaruka na kuungana (vikawa kitu kimoja) na kuwa kisahani KIMOJA kinachoruka, cha ukubwa uliokuwa sawa. Kisha bila kutarajia Ngumi ya Bwana ikajitokeza kutoka Mbinguni pamoja na NGUVU KUU na kuitwanga sahani ile iliyokuwa inaruka angani katikati na kuiangusha chini, kutoka angani. (Mwisho). Unabii: Bwana akasema, "Yote yale uyaonayo ni Ukweli na Yanaaminika." (Mwisho). Maono: Bwana alinionyeshea joka fulani mkubwa na mkia wake ukiwa unaenda juu na chini pole pole utadhani ni mkwaju au kiboko. (Mwisho). Maono: Mimi nilionyeshewa boti mbili aina ile ya mashindano, zikienda kasi zikiwa zinaenda ubavu kwa ubavu juu ya maji. (Mwisho). Maono: Niliona tena kichwa cha joka mkubwa. (Mwisho). Maono: Niliona volkano fulani kubwa sana ikiwa na mawe yaliyoyeyuka humo ndani. (Mwisho). Maono: Bwana alinionyeshea piramidi iliyokuwa imewekwa kichwa chini ikiwa imekalia kwenye ncha yake (au kwenye kilele chake). (Mwisho). Maono: Bwana alinionyeshea buibui fulani wa ajabu ambaye ni mkubwa mweusi na mwenye manywele na mwili wake ukiwa umepasuliwa. Kisha mwili uliokuwa na rangi ya bluu-kijani ukaonekana kutoka kwenye katikati ya ngozi ya mwili huo. (Mwisho). Unabii: Bwana akasema, "Angalia na ujifunze." (Mwisho). Maono: Kisha mimi niliona maono ya moyo tena, lakini moyo huo ulikuwa umekamilika. Wakati nikiwa ninaungalia niliona kidole juu ya moyo huo, pale moyo unapoungana. (Mwisho). Unabii: Kisha Bwana aksema, "Ufalme wa Mungu uko mbele yenu." (Mwisho). Maono: Mimi niliona ukuta wa barafu na ulikuwa unaonekana ukiwa unasogea. (Mwisho). Maono: Mimi niliona madaraja ya aina ya kuegeshwa yakiwa yako ubavu kwa ubavu. (Mwisho). Maono: Kisha mimi nikaona sahani au beseni kubwa lakini iliyokuwa tambarare kabisa ikiwa na fimbo au ubao uliokuwa bapa umewekwa katikati yake, lakini ukiwa juu ya beseni hiyo. Wakati nikiwa ninauangalia hivi,niliona mshumaa mweupe unaowaka ukiwa umewekwa juu ya ubao huo, sehemu ya katikati yake. (Mwisho). Maono: Mimi niliona mlima fulani mkubwa ambao umekatwa nusu mviringo mkubwa kwenye kitako chake. Nusu mviringo huo ulikuwa mkubwa kiasi ambacho ulikuwa umeenda theluthi mmoja ya mlima huo. Ulikuwa unaweza kuona kupitia kwenye tako la mlima huo kwa sababu ya nusu mviringo huo, na katikati ya nusu mviringo huo uliokuwa kama handaki, kulikuwa na ubao mkubwa sana ulio kwenda ndani ya mlima huo na kwenda kupitia kwenye handaki hilo la nusu mviringo. Na ubao huo ulikuwa umewekewa uzito kila upande kama mfano wa bembea ya watoto ya kwenda juu na chini nami nikawa ninaiona ikienda juu chini. (Mwisho). Maono: Bwana alinionyeshea frampeni ya chuma ya udongo nyeusi iliyojazwa mkaa uliokuwa mwekundu. Nilivyokuwa naiangalia kwa makini hiyo frampeni, ikawa imesogezwa umbali wa futi chache na mkaa huo uliokuwa umekuwa mwekundu kwa moto ukamwagwa kwenye chungu fulani kikubwa. Haya yalitokea mara nyingi kidogo wakati mimi nikiwa ninauangalia. (Mwisho).
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )