|
896. Vision
given to Raymond Aguilera on 10 April 1996 at 8:30 PM. During prayer and worship the Lord showed me a bowl that was going to be carved with wide flat putty knife and I wondered how can the Lord carve this bowl with this wide putty knife? So I asked the Lord, "How can this wide flat putty knife carve into this curved bowl? Then before my eyes the Lord transformed the wide putty knife into a curved chisel that would be ideal for curving the curved surface of the bowl. Vision: Then the Lord showed me a vision of a bunch of small colorful flowers sticking out of this large and long braided flat basket that looked like a two foot long flat purse. Vision: A vision of a metal construction safety hard hat. Then I saw a hack saw cut it in two from the top across the width. (above and across where the ears are located.) Vision: The next image was of a hangman's noose hanging from this horizontal brace. This brace and hangman's noose were on this pier next to the water. Then this fish with enormous teeth jumped out of the water and bit the noose and ripped it off the brace and took it into the water.
|
896. Maono
aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 10 Aprili 1996 saa 2:30 usiku. Wakati wa maombi na kuabudu Bwana alinionyeshea bakuli ambalo linaenda kuchongwa kwa kisu bapa ambacho huwa kinatumika kupakalia au kukwangulia rangi au puti, nami nikawa najiwazia itawezekaneje kwa Bwana kukitumia kisu hicho cha kuwekea puti kuchongea bakuli? Mimi Nikamwuliza Bwana, "Kisu hicho bapa na kipana kitawezeje kuchonga kisahani hicho cha mviringo? Kisha Bwana mbele ya macho yangu alikigeuza hicho kisu kipana cha kupakaa puti na kuifanya kuwa na muundo uliojipinda kama patasi, ambayo inafaa kuchongea uso wa bakuli hilo. Maono: Kisha Bwana alinionyeshea maono ya rundo la maua madogo madogo yenye rangi nyingi nzuri zikiwa zinajitokeza kutoka kwenye kapu fulani ndefu iliyo tariziwa ambayo ilikuwa inaonekana kama puchi kubwa ya urefu wa futi mbili. Maono: Maono ya kofia ngumu ya chuma itumikayo kwenye ujenzi. Kisha msumeno ukakikata kofia hicho vipande viwili kuanzia juu hadi kwenye mapana yake. (ili katwa kwenye eneo la usawa wa masiko.) Maono: Maono yaliyofuata yalikuwa ni ya kamba ya mnyongaji ikiwa ina ning’inia kutoka kwenye boriti la chuma lililokuwa limelala kwa usawa. Boriti hiyo pamoja na kamba hiyo ya mnyongaji ilikuwa juu ya nguzo karibu na maji. Kisha samaki fulani aliyekuwa na meno makubwa sana; aliruka kutoka kwenye maji hayo na kuking’ata kamba hiyo na kuitoa kutoka kwenye boriti hiyo na kuzama nayo majini.
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )